Wednesday, July 13, 2011

MBUNGE WA IGUNGA AJIVUA GAMBA RASMI LEO.



Mbunge wa Igunga na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi NEC kupitia mkoa wa Tabora Rostam Aziz siku hii ya leo kwa ridhaa yake ametangaza kujiuzulu na kuachia ngazi katika nyadhifa zote alizokuwa nazo kama mjumbe wa Nec na Mbunge wa igunga,

Tamko hilo amelitoa siku hii ya leo majira ya saa tisa alasiri katika Ukumbi wa Sakao huko Igunga tabora...

Baada tu ya kutoa Tamko hilo wananchi waliokuwa eneo hilo walionekana kutoridhishwa kabisa na maamuzi hayo yaliyotolewa na kuonekana wazi kabisa wakipinga huku wakisema ''HATUTAKI" wakipinga uamuzi huo uliotolewa kwa kumtaka aendelee kuwepo kwenye nyadhifa hizo ambapo mbali na kuwa Mbunge pia alikuwa mjumbe wa NEC.

Rostam alikuwa ni mbunge wa IGUNGA kwa mda wa miaka 18 na alikuwa ni mjumbe wa NEC kwa Awamu tatu mfululizo.

Friday, June 24, 2011

BINTI MWENYE ULIMI MREFU DUNIANI


Binti Annika Irmler (pichani juu) ambaye ni raia wa Ujerumani ana umri wa miaka 16 ndiye mwanamke mwenye ulimi mrefu zaidi duniani kwa mujibu wa Kitabu cha Rekodi za Dunia za Guinness.

Binti huyo ambaye alivunja rekodi hiyo mwaka 2007 ni mwanafunzi wa sekondari, wakati huo alipokuwa anavunja rekodi alikuwa umri wa miaka 12.

Kwa ufahamu zaidi, mrembo Annika ana ulimu wenye urefu wa sentimita 7.6.  Utakuwa huna ubishi kama utatazama picha inayoonyesha kipimo hicho.

Annika anasema: “Sijui sana kuhusu ndimi, huenda ulimi wangu ukaendelea kurefuka.  Hata hivyo, nafurahi walimwengu wengi wananifahamu sasa kupitia ulimi huu.”

Kwa kina kaka na kina dada wanaopenda kurefusha ndimi zao, nafikiri teknolojia ya sasa inawezesha hivyo, kwani kuna utaalam mwingi tu wa kukuza viungo vingi vya mwili.
Kujaribu si vibaya, kwani kutojaribu ni kushindwa tayari. hahahahahahahahaaaaaaaaaaaaa!..... yangu macho ngoja nitafute na mwanaume aliyevunja rekodi.

Tuesday, June 21, 2011

FAIDA 5 ZA WAPENZI KUNUNIANA!..




Yaweza kuwa ni mada ambayo imekuacha hoi mpenzi msomaji wangu huku ukijiuliza kama ni kweli zipo faida kwa watu wanaopendana kwa dhati kununiana.

Faida ipi hiyo zaidi ya maumivu na mateso ya moyo? Jamani ni kweli kabisa kwamba kuna maumivu na karaha nyingi unaponuniana na mpenzi wako, lakini wakati huo huo kuna faida nyingi za kununiana naye.

Mapenzi yana wigo mpana mno ambao mtu anapaswa kuuangalia kwa jicho pana na akili pembuzi kabla ya kuingia, namaanisha kwamba ni lazima kuchunguza kina cha maji kabla ya kuzamia. Sasa basi, zifuatazo ni faida tano utakazozipata ukiwa umenuniana na mpenzi wako.

HUSAIDIA KUPUNGUZA MIGOGORO


Ni ukweli usiopingika kuwa, katika hali ya kawaida, ukiwa mbali na mtu fulani katika jamii unayoishi ni vigumu sana kujikuta umekwaruzana naye. Hii ni kwasababu utakuwa hauingiliani naye katika mizunguko yako, vivyo hivyo kwa wapenzi walionuniana.

Hali hii hupunguza kabisa migogoro ya hapa na pale, kwani hiki ni kipindi ambacho mtakuwa mbalimbali jambo ambalo huepusha maudhi ya kibinadamu.

Mfano, yawezakana katika kipindi mlichonuniana na mpenzi wako, uliingia ujumbe wa mapenzi kwenye simu yake kutoka kwa mtu aliyekosea namba. Kwa kuwa hauko naye karibu jambo hili halitakuumiza maana hutaelewa nini kimeendelea tofauti na kama ungelikuwa naye karibu.

Kwa hiyo kuna baadhi ya maumivu na maudhi ambayo utaepukana nayo kwa kipindi cha kununiana kwenu. Ni kweli kabisa kwamba hupunguza migogoro na mitafaruku ya hapa na pale, umeelewa mpenzi msomaji wangu? Haya twende kwenye faida ya pili.

KUBAINI TABIA X ZA MWENZAKO

Hiki ni kipindi ambacho sasa kitakusaidia wewe kubaini tabia na mienendo mibaya ya mwenzi wako. Hii ni kwa kuwa utakuwa mbali naye hivyo naye hujiona kuwa yuko huru kufanya jambo lolote analoona kuwa linafaa bila kujali uwepo wako kwani kila mtu hana ‘time’ na mwenzake.

Kama kuna asili ya maisha yake ambayo aliiacha baada ya kuingia katika uhusiano na wewe, ambayo ni mbaya zaidi sasa hapa ataanza kuirudia kwa kujiona kuwa hana mtu wa kumzuia na kumbana.

Kama ni mlevi kupindukia, mchafu, muongo na tabia nyingine mbaya za kufanana na hizi basi ataanza kuzionesha katika kipindi ambacho mmenuniana.

KUPATA MUDA WA KUTAFAKARI ZAIDI

Hapa naomba nieleweke vizuri kabisa kwamba, ninapoongelea suala la kutafakari zaidi katika kipindi ambacho wewe hauna maelewano mazuri na mwenzi wako, namaanisha kuwa utapata muda mzuri zaidi wa kutafakari penzi lenu kwa ujumla.

Ni kipindi kitachokuongoza wewe kuwa na uelewa wa ni aina gani ya mpenzi uliyenaye. Kivipi? Ni kwamba, katika muda huu mara nyingi utataka kupata suluhu ya kununiana kwenu, lakini pia katika kutafuta suluhu hiyo utapata fursa ya kutafakari kwa kina juu ya penzi lenu huku ukimpima mwezi wako kwa mtazamo chanya.


KUFAHAMU AINA YA MARAFIKI ZAKE 


Si kila rafiki wa mwenza wako ana nia nzuri na uhusiano wenu au anafurahia penzi lenu. Mathalani, labda wewe ni msichana na pengine miongoni mwa rafiki zake kuna mmoja au wawili ambao hutamani sana kupata penzi lako.

Sasa katika kipindi ambacho utakuwa umenuniana na mpenzi wako basi itakuwa ni nafasi nzuri kwao kuitumia kunyunyizia sumu ya kumponda huku wakikutamkia maneno ya kukushawishi, hivyo utakuwa umeelewa ni aina gani ya marafiki alionao mwenzi wako.

Hii si kwa msichana tu, hata kwa wanamume kwani huenda kati ya rafiki wa ‘girlfriend’ wako, kuna wanaokutamani, sasa wakiona huna uhusiano mzuri na mpenzi wako, watatumia nafasi hii kukuambia maneno ya uongo juu yake na kukuonesha kila dalili za kukutaka.
Hivyo utakuwa umefahamu ni aina gani ya rafiki ambao mpenzi wako anao. Tambua kwamba, marafiki wengi wana tabia zinazofanana.


KUBAINI AINA YA PENZI ALILONALO KWAKO

Katika kipindi hiki, utaweza kuelewa ni aina gani ya penzi alilonalo huyo mtu wako juu yako. Kwa mpenzi aliye na hisia za dhati kabisa kwako, katika kipindi hiki atakuwa ni mtu wa kutafuta njia ya kupata suluhu ya tatizo lenu.

Pamoja na kwamba wewe utakuwa umenuna, bado yeye ataonesha kukujali kama kawaida, atakupigia simu za hapa na pale yaani ilimradi tu asikie angalau sauti yako, lengo lake likiwa ni kutaka kurejesha ukaribu ambao sasa anaona kama akiupoteza itakuwa ni maumivu kwake.

Kwa mantiki hiyo basi, utagundua ni kwa jinsi gani anathamini penzi lenu na ni aina gani ya penzi alilonalo kwako. Yote haya utabahatika kuyajua kupitia kipindi cha kununiana kwenu.

Hata hivyo, niwatahadharishe kwamba, kuandika haya isiwe ni tiketi ya wewe sasa kuanza kununiana na mpenzi wako eti kwa kigezo kwamba utapata nafasi ya kumfahamu, la hasha!
Siku zote katika uhusiano wako epuka maudhi na migogoro isiyokuwa ya lazima.

Naamini somo limekuingia vizuri, sasa jiandae kupata mada nyingine kali zaidi.
Tchao!

Tuesday, June 14, 2011

WANYAMA WENYE SURA MBAYA DUNIANI

Duniani kuna wanyama ambao wana sura mbaya sana, na hii ni top 5 list ya wanyama hao wenye sura mbaya.
wa kwanza ni


huyu anaitwa Daubentonia madagascariensis anapatikana katika kisiwa cha Madagascar ambaye ana mchanganyiko wa meno kama ya panya na kidole chembamba cha kati ili kukamilisha uwepo wake kimazingira kama gogota. Ni aina kubwa ya nyani duniani kati ya wanyama wanaotembea usiku mwenye sifa ya  kipekee ya kupata chakula kwa kuchimba miti ama kuingiza vidole vyake katika matundu yaliyoko kwenye miti na kutafuna. Ana uzito wa kilo 2.5, na majike wana uzito pungufu kidogo (kwa wastani wa gramu 100) ukilinganisha na madume. Mbali na uzito na viungo vya jinsia macho yao hayadhihirishi jinsia. Wote hukua kutoka cm 30-37 kutoka kichwa na mwili, na mkia 44-53 cm.

wa pili ni


huyu anaitwa Sphynx Cat Canada asiye na manyoya ni aina nadra sana ya paka na mwenye manyoya kidogo saaana, kwa maana nyingine manyoya mafupi saana juu ya mwili wake. Ngozi yao ni kama rangi ya manyoya yao, na paka wote kawaida huashiria mwelekeo (imara, uhakika, kasi, n.k). Wakati mwingine hufananishwa kimakosa na Chihuahuas kwa sababu ya muonekana wao ufananao na paka. Wao wana akili sana, wenye kujiamini na wapole, mara nyingi hupenda kukumbatia wamiliki wao, binadamu wengine, na wenyewe kwa wenyewe.


wa tatu ni

huyu anaitwa Babirusa au nguruwe-deer ni mnyama mwenye muonekano kama wa nguruwe anaepatikana maeneo ya Sulawesi na visiwa jirani vya Indonesia. Kwa kawaida Babirusa huwekwa kwenye kundi la aina moja ya Babyrousa, lakini utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kwamba kuna aina kadhaa zinazoweza kutofauitshwa kwa msingi wa jiografia, ukubwa wa mwili, kiasi cha nywele mwilini, na sura ya meno ya juu kwa madume.

wa nne ni

huyu anaitwa Viperfish (aina ya Chauliodus) ni samaki wa kina kirefu cha maji mwenye meno marefu kama sindano yanayochomoza toka taya ya chini. Hukua kwa urefu wa sentimita 30 hadi 60 (14 inches). Jina Viperfish pia wakati mwingine kutumiwa na weever mdogo

wa tano ni

huyu anaitwa Anglerfish, historia yake bado sijaijua sawasawa ila nawaahidi kuwa nafuatilia historia yake na mara nitakapoipata nitawawekea.

Saturday, June 11, 2011

BHOKE BBA.

Huyu mtoto jamani yani hata mshipa wa aibu hana kabisa kabisa, halafu eti anasema haregret hata kidogo aliyoyafanya kwani BBA alienda kujiwakilisha mwenyewe na wala hakuenda kumuwakilisha mtu. Mmmmmmmmmmh!... Tuwe na aibu jamani, kweli huyu mtoto kashindikana... Bhoke umetuaibisha sana, Wakurya andamaneni!...


NYIMBO NINAZOZIPENDA NA NITAZIPENDA DAIMA.

kama nawe unazifeel hizi nyinmbo basi karibu tuburudike kwa pamoja. Kwa Kweli hizi nyimbo nazipenda sana na huwa napenda kuzisikiliza mara kwa mara. karibu tuburudike



All I Have by JLO & L L Cool J, I real Love it.


We Belong Together by MAria Carey.

Tuesday, June 7, 2011

SAFARI YA MWISHO YA NDUGU YETU JOSHUA MWASOMOLA.

Ndugu yetu Joshua Lefson Mbalekile Mwasomola alizaliwa mwaka 1961 huko Tukuyu Mbeya na amefariki dunia tarehe 02/06/2011 saa nne usiku katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
Mwasomola alikuwa akiishi Mkoani Tanga lakini alikuwa akifanya kazi Makambako ambako alikuwa akifanyia kampuni ya Lima Limited kama Assistant Warehouse Manager. Marehemu amefariki kwa kuugua kisukari na pressure.
Marehemu ameacha mjane na watoto wanne, wa kike mmoja na wa kiume watatu. Tulimpenda sana lakini mungu kampenda zaidi.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMENI.



Ndugu Joshua Mwasomola kama mnavyomuona kwenye picha enzi za uhai wake.


Mchungaji Peter Mgeni akuiombea mwili wa marehemu kabla ya kumzika, Marehemu alikuwa akisali katika dhehebu la Moravian.


Mwili wa marehemu ukishushwa kwenye gari mara baada ya kufika Ushirika Tukuyu tukitokea Mbeya alikofia.


Kushoto aliyevaa nguo ya light blue ni jirani na aliyekuwa anasali na marehemu mwasomola katika dhehebu la Moravian huko Mkoani Tanga, kwa hiyo huyu mama alisafiri toka Tanga kuja kumzika jirani yake, Ndugu yetu mwasomola.
Anaefuatia toka kushoto aliyevaa T-shirt Nyeupe na kitambaa cheupe kichwani ni Mke wa marehemu (Mjane aliyeachwa na marehemu.) mama Abraham.
Bibi anayefuatia aliyevaa kitambaa cheusi kichwani ni mama mzazi wa marehemu, inasikitisha sana tena sana.


Mama Kutoka Tanga akisali kufungua misa ya marehemu ili iweze kuanza.


Huyo aliyesuka Yeboyebo kainama, ni mtoto wa kaka ya marehemu, yani marehemu ni baba mdogo wake, lakini wameishi nae toka kitambo sana, sasa alikuwa na uchungu mkubwa sana tena sana kwa kuondokewa na baba.


Marehemu Mwasomola kwenye Jeneza.


Kabuli lililoandaliwa la kumpumzisha ndugu Joshua Mwasomola.






Watoto wa Marehemu Joshua Mwasomola wakiweka Mashada kwenye kaburi la mpendwa baba yao.

Monday, June 6, 2011

KIKOMBE CHA BABU CHAFIKA KWA OBAMA MMMMMMMMMMMH!.......

Duh kweli babu noma hebu cheki hiyo. Obama naye aamua kwenda kula Kikombe halafu analipa kwa dola, Ndio ujue kuwa babu yupo juuuuuuuuuuuuuuu!..



Thursday, May 26, 2011

Lima Limited Mbinga



Hii kama inavyoonekana ni ofisi la Lima Limited Mbinga, Kampuni ya kununua kahawa, kwa chini ni ofisi na juu ni vyumba wanavyolala wafanyakazi wanaofanya kazi katika kampuni hii.
Camera yangu iliniishia charge na bahati mbaya sikutembea na charger hivyo sikuweza kupiga picha nyingi zaidi.


Nje ya ofisi kuna uwanja mkubwa sana pamoja na kiwanda kwa pembeni, ila nawaahidi next time nikienda nitapiga picha za kiwandani kwenye vichanja ili muweze kuona mambo ya kahawa yanatokana na nini, hayo muyaonayi ni magali mali ya Lima Limited, ya kusombelea kahawa.



Kahawa kama mnavyoiona.



Ila bado haijaiva lakini ndio inaelekea kuiva. na ikiiva inakuwa nyekundu kabisa.


Last week nilipata fursa ya kutembelea Mkoa wa Ruvuma wilaya ya mbinga.

Kwa kweli mbinga kumejaaliwa kuwa na kahawa kwa wingi sana tena sana, na kuna makampuni mengi yanayonunua kahawa kama Lima Limited, Tutunze, Dae LTD na mengineyo. kwa hiyo ushindani ni mkubwa kwa kiasi fulani ukiangalia kuna kata kichwa pia.

Safari yetu ilikuwa nzuri sana, kwa kweli toka songea kwenda mbinga ni mwendo kama wa dk 45 lakini kutokana na barabara kuwa mbaya hasa wakati wa masika mmmmmmmmmmmmh!... utatumia hata zaidi ya masaa mawili, lakini kwa bahati nzuri watu wa mbinga wamekumbukwa maana tumekuta wachina wapo busy ile mbaya kutengeneza bara bara, na wameitanua sana sana yani niliipenda kwa kweli.



Duu huyu mchina sijui amechoka na kazi maana alikuwa anasinzia tu,



Hili ndio karavati kama linavyoonekana, jamaa wanapiga kazi hawa balaa, usiku na mchana, hawataki mchezo.






Hapo mchina yupo makini kuangalia wanavyoweka mafuta maana anajua Tanzania kila kitu ni ufisadi tu sasa wabongo wasije wakamchakachua mafuta. yupo makini huyo.




 Hii mashine sikufanikiwa kuipiga yote ikaonekana, haraka harak tena, ila ilikuwa inangoa mti na visiki, anazamisha vyuma chini akiinua basi mti umeng'oka, niliipenda kwa kweli, sio wabongo wanang'ang'ana na sululu hadi mikono inaota sugu.




Hili ni eneo lililotengwa kwa ajili ya kuweka mizani, Mbinga kuna kahawa nyingi sana, sasa baada ya ununuzi huwa wanasafirisha kupeleka makambakona baada ya hapo ndipo husafirishwa kupelekwa nje ya nchi au mnadani moshi. kwa sababu hiyo basi wa mizani wameona kama ni vema wakaweka mizani katika wilaya hiyo ya mbinga. Big up mbunge wa mbinga maana umefanya kitu cha maana sana, nimeipenda kwa kweli.
Shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Captain John Komba.

Friday, May 20, 2011

BREAKING NEEEEEEWZ!.... SHEHE YAHYA HATUPO NAYE TENA



Kwa taarifa zilizotufikia mchana huu ni kwamba, Mtabiri mahiri na maarufu aliyewahi kutabiri katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana kuwa kiongozi mkubwa angefariki dunia kabla ya uchaguzi na kweli alifariki mgombea mwenza wa chama cha chadema. Amefariki dunia

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi maana hakika tutamkumbuka kwa utabiri wake maana pia aliwahi kutabiri mambo mengi sana ikiwemo ya Simba kufungwa na Yanga na kweli ilikuwa hivyo.

MAY GOD REST HIM IN PEACE... AMEN

Wednesday, February 23, 2011

 Uncle JJ ndani ya pozi la picha.


 Mzazi na mfugo wake katika pozi.





 Jirani jamani.. si unajua tena mambo ya uswazi.





 mama mama mama, mama, mama huyo!.. mama mama mama mama mama huyo mama mama mama huyo






Pozi hilo baada ya watu kuvimbiwa Pilau. mazagazaga,




 dogo na pozi la kazi.




aaaaaaaaah, jama dogo furaha ilimzidi hadi akaamua kulala chini!... mmhhhhhhhhhh

MY Dady Birthday

 Baba na mama (Wazazi hao). mama kazika pozi wakati wa birthday ya mmewe alipotimiza miaka 81, can you imagine jamani. wakati sisi sasa hivi tunakufa vijana wadogowadogo... nazidi kumuombea baba yangu azidi kuishi maisha mengine marefu zaidi.

 Familia na majirani katika sherehe ya mazi jamani.mama kwa pembeni upande wa kulia akifuatiwa na wakwe zake, na akifuatiwa na braza jamani/ anaefuata ni jirani waribu sana na wengineo.

 Likeki hiloooooooooooo, na yale mambo yetu mmmmmmmmmmmmmmmmh!... ilinoga jamani.
japo kalikuwa kasmall function lakini ilifurahisha kwa kweli.


wazazi na mwanao mkubwa kidogo sio mkubwa snaa, nadhani mmenielewa nilichomaanisha.


 Wazazi na mkweo jamano!.








Hi to all, poleni jamani kwa kimya kirefu... i was a bit busy dats y hata kuingia kuwablogisha ikawa ngumu kidogo... bt am free now