Thursday, May 26, 2011

Lima Limited Mbinga



Hii kama inavyoonekana ni ofisi la Lima Limited Mbinga, Kampuni ya kununua kahawa, kwa chini ni ofisi na juu ni vyumba wanavyolala wafanyakazi wanaofanya kazi katika kampuni hii.
Camera yangu iliniishia charge na bahati mbaya sikutembea na charger hivyo sikuweza kupiga picha nyingi zaidi.


Nje ya ofisi kuna uwanja mkubwa sana pamoja na kiwanda kwa pembeni, ila nawaahidi next time nikienda nitapiga picha za kiwandani kwenye vichanja ili muweze kuona mambo ya kahawa yanatokana na nini, hayo muyaonayi ni magali mali ya Lima Limited, ya kusombelea kahawa.



Kahawa kama mnavyoiona.



Ila bado haijaiva lakini ndio inaelekea kuiva. na ikiiva inakuwa nyekundu kabisa.


Last week nilipata fursa ya kutembelea Mkoa wa Ruvuma wilaya ya mbinga.

Kwa kweli mbinga kumejaaliwa kuwa na kahawa kwa wingi sana tena sana, na kuna makampuni mengi yanayonunua kahawa kama Lima Limited, Tutunze, Dae LTD na mengineyo. kwa hiyo ushindani ni mkubwa kwa kiasi fulani ukiangalia kuna kata kichwa pia.

Safari yetu ilikuwa nzuri sana, kwa kweli toka songea kwenda mbinga ni mwendo kama wa dk 45 lakini kutokana na barabara kuwa mbaya hasa wakati wa masika mmmmmmmmmmmmh!... utatumia hata zaidi ya masaa mawili, lakini kwa bahati nzuri watu wa mbinga wamekumbukwa maana tumekuta wachina wapo busy ile mbaya kutengeneza bara bara, na wameitanua sana sana yani niliipenda kwa kweli.



Duu huyu mchina sijui amechoka na kazi maana alikuwa anasinzia tu,



Hili ndio karavati kama linavyoonekana, jamaa wanapiga kazi hawa balaa, usiku na mchana, hawataki mchezo.






Hapo mchina yupo makini kuangalia wanavyoweka mafuta maana anajua Tanzania kila kitu ni ufisadi tu sasa wabongo wasije wakamchakachua mafuta. yupo makini huyo.




 Hii mashine sikufanikiwa kuipiga yote ikaonekana, haraka harak tena, ila ilikuwa inangoa mti na visiki, anazamisha vyuma chini akiinua basi mti umeng'oka, niliipenda kwa kweli, sio wabongo wanang'ang'ana na sululu hadi mikono inaota sugu.




Hili ni eneo lililotengwa kwa ajili ya kuweka mizani, Mbinga kuna kahawa nyingi sana, sasa baada ya ununuzi huwa wanasafirisha kupeleka makambakona baada ya hapo ndipo husafirishwa kupelekwa nje ya nchi au mnadani moshi. kwa sababu hiyo basi wa mizani wameona kama ni vema wakaweka mizani katika wilaya hiyo ya mbinga. Big up mbunge wa mbinga maana umefanya kitu cha maana sana, nimeipenda kwa kweli.
Shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Captain John Komba.

Friday, May 20, 2011

BREAKING NEEEEEEWZ!.... SHEHE YAHYA HATUPO NAYE TENA



Kwa taarifa zilizotufikia mchana huu ni kwamba, Mtabiri mahiri na maarufu aliyewahi kutabiri katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana kuwa kiongozi mkubwa angefariki dunia kabla ya uchaguzi na kweli alifariki mgombea mwenza wa chama cha chadema. Amefariki dunia

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi maana hakika tutamkumbuka kwa utabiri wake maana pia aliwahi kutabiri mambo mengi sana ikiwemo ya Simba kufungwa na Yanga na kweli ilikuwa hivyo.

MAY GOD REST HIM IN PEACE... AMEN