Wednesday, July 13, 2011

MBUNGE WA IGUNGA AJIVUA GAMBA RASMI LEO.



Mbunge wa Igunga na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi NEC kupitia mkoa wa Tabora Rostam Aziz siku hii ya leo kwa ridhaa yake ametangaza kujiuzulu na kuachia ngazi katika nyadhifa zote alizokuwa nazo kama mjumbe wa Nec na Mbunge wa igunga,

Tamko hilo amelitoa siku hii ya leo majira ya saa tisa alasiri katika Ukumbi wa Sakao huko Igunga tabora...

Baada tu ya kutoa Tamko hilo wananchi waliokuwa eneo hilo walionekana kutoridhishwa kabisa na maamuzi hayo yaliyotolewa na kuonekana wazi kabisa wakipinga huku wakisema ''HATUTAKI" wakipinga uamuzi huo uliotolewa kwa kumtaka aendelee kuwepo kwenye nyadhifa hizo ambapo mbali na kuwa Mbunge pia alikuwa mjumbe wa NEC.

Rostam alikuwa ni mbunge wa IGUNGA kwa mda wa miaka 18 na alikuwa ni mjumbe wa NEC kwa Awamu tatu mfululizo.