Thursday, May 26, 2011

Last week nilipata fursa ya kutembelea Mkoa wa Ruvuma wilaya ya mbinga.

Kwa kweli mbinga kumejaaliwa kuwa na kahawa kwa wingi sana tena sana, na kuna makampuni mengi yanayonunua kahawa kama Lima Limited, Tutunze, Dae LTD na mengineyo. kwa hiyo ushindani ni mkubwa kwa kiasi fulani ukiangalia kuna kata kichwa pia.

Safari yetu ilikuwa nzuri sana, kwa kweli toka songea kwenda mbinga ni mwendo kama wa dk 45 lakini kutokana na barabara kuwa mbaya hasa wakati wa masika mmmmmmmmmmmmh!... utatumia hata zaidi ya masaa mawili, lakini kwa bahati nzuri watu wa mbinga wamekumbukwa maana tumekuta wachina wapo busy ile mbaya kutengeneza bara bara, na wameitanua sana sana yani niliipenda kwa kweli.



Duu huyu mchina sijui amechoka na kazi maana alikuwa anasinzia tu,



Hili ndio karavati kama linavyoonekana, jamaa wanapiga kazi hawa balaa, usiku na mchana, hawataki mchezo.






Hapo mchina yupo makini kuangalia wanavyoweka mafuta maana anajua Tanzania kila kitu ni ufisadi tu sasa wabongo wasije wakamchakachua mafuta. yupo makini huyo.




 Hii mashine sikufanikiwa kuipiga yote ikaonekana, haraka harak tena, ila ilikuwa inangoa mti na visiki, anazamisha vyuma chini akiinua basi mti umeng'oka, niliipenda kwa kweli, sio wabongo wanang'ang'ana na sululu hadi mikono inaota sugu.




Hili ni eneo lililotengwa kwa ajili ya kuweka mizani, Mbinga kuna kahawa nyingi sana, sasa baada ya ununuzi huwa wanasafirisha kupeleka makambakona baada ya hapo ndipo husafirishwa kupelekwa nje ya nchi au mnadani moshi. kwa sababu hiyo basi wa mizani wameona kama ni vema wakaweka mizani katika wilaya hiyo ya mbinga. Big up mbunge wa mbinga maana umefanya kitu cha maana sana, nimeipenda kwa kweli.
Shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Captain John Komba.

1 comment:

  1. Play Slots Online - Dr.MD
    Learn 태백 출장샵 how to play slot machines online in Michigan by using our 사천 출장안마 guide, 제주 출장안마 demo 동해 출장마사지 play guide and how to 충청북도 출장안마 win real money playing online slots for real money. Dr

    ReplyDelete