Tuesday, June 7, 2011

SAFARI YA MWISHO YA NDUGU YETU JOSHUA MWASOMOLA.

Ndugu yetu Joshua Lefson Mbalekile Mwasomola alizaliwa mwaka 1961 huko Tukuyu Mbeya na amefariki dunia tarehe 02/06/2011 saa nne usiku katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
Mwasomola alikuwa akiishi Mkoani Tanga lakini alikuwa akifanya kazi Makambako ambako alikuwa akifanyia kampuni ya Lima Limited kama Assistant Warehouse Manager. Marehemu amefariki kwa kuugua kisukari na pressure.
Marehemu ameacha mjane na watoto wanne, wa kike mmoja na wa kiume watatu. Tulimpenda sana lakini mungu kampenda zaidi.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMENI.



Ndugu Joshua Mwasomola kama mnavyomuona kwenye picha enzi za uhai wake.


Mchungaji Peter Mgeni akuiombea mwili wa marehemu kabla ya kumzika, Marehemu alikuwa akisali katika dhehebu la Moravian.


Mwili wa marehemu ukishushwa kwenye gari mara baada ya kufika Ushirika Tukuyu tukitokea Mbeya alikofia.


Kushoto aliyevaa nguo ya light blue ni jirani na aliyekuwa anasali na marehemu mwasomola katika dhehebu la Moravian huko Mkoani Tanga, kwa hiyo huyu mama alisafiri toka Tanga kuja kumzika jirani yake, Ndugu yetu mwasomola.
Anaefuatia toka kushoto aliyevaa T-shirt Nyeupe na kitambaa cheupe kichwani ni Mke wa marehemu (Mjane aliyeachwa na marehemu.) mama Abraham.
Bibi anayefuatia aliyevaa kitambaa cheusi kichwani ni mama mzazi wa marehemu, inasikitisha sana tena sana.


Mama Kutoka Tanga akisali kufungua misa ya marehemu ili iweze kuanza.


Huyo aliyesuka Yeboyebo kainama, ni mtoto wa kaka ya marehemu, yani marehemu ni baba mdogo wake, lakini wameishi nae toka kitambo sana, sasa alikuwa na uchungu mkubwa sana tena sana kwa kuondokewa na baba.


Marehemu Mwasomola kwenye Jeneza.


Kabuli lililoandaliwa la kumpumzisha ndugu Joshua Mwasomola.






Watoto wa Marehemu Joshua Mwasomola wakiweka Mashada kwenye kaburi la mpendwa baba yao.

No comments:

Post a Comment